Mlinzi akamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha uhalifu kupitia WhatsApp

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema limemkamata na linaendelea kumshikilia Ambrose Leonce Dede ambaye mi mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya African Safari na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha uhalifu nchini kupitia kundi la WHATSAPP lijulikanalo kwa jina la SAUTI YA WATANZANIA.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Msemaji wa Jeshi la Polisi makao Makuu ya Polisi Dodoma,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,mtuhumiwa alikamatwa akiwa maeneo ya njia panda ya Makiungu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Kulingana na ushahidi uliokusanywa kabla na baada ya kukamatwa kwake, unaonesha katika kundi hilo yupo pamoja na wasimamizi wengine wa kundi hilo la whatsApp (Group Admin’s) na wanashirikiana na baadhi ya watu waliopo nchini na wengine wakiwa nje ya mipaka ya nchi yetu.

Alioshirikiana nao kupanga, kuendelea kupanga na kuhamasisha uhalifu nchini kwa mwavuli wa maandamano ya amani ni pamoja na wanaotumia namba zifutazo;

+44746913055
+46732533609
+1(240)423-3331
+44784821186
+1(649)9348015
+255758000000
+255655684245

"Uchunguzi unakamilishwa ikiwa ni pamoja na kuwapata wengine anaoshiriana nao na wanatumia namba ambazo hatujazitaja kwa sababu za kiuchunguzi na ukamataji. Baada ya kukamilisha hayo hatua zingine za kisheria zitafuata.

"Jeshi la Polisi, linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujihusisha na makundi ya mawasiliano mtandaoni yanayoendeshwa na watu waliopanga na wanaendelea kupanga kufanya uhalifu nchini kwa mwavuli wa maandamano ya amani au kwasababu nyingine yeyote ile kwani huo ni uhalifu na hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria bila kumwonea muhali yeyote yule atakayebainika.

"Aidha, ni vizuri kila mmoja wetu kutambua kuwa, watu wa aina hiyo wanaopanga na kuhamasisha uvunjifu wa amani, wanaoumia ni sisi Watanzania wakati wao na familia zao hawapati madhara yoyote na wanaendelea kunufaika na fedha wanazolipwa kupitia makundi ya mawasiliano mtandaoni wanayoyaanzisha na kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here