DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza S. Johari ameshiriki hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hafla hiyo imefanyika leo Novemba 14,2025, Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

