DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amehudhuria sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji George Mcheche Masaju, amemwapisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba, kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Sita baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Sherehe hizo pia zimeambatana na kuapishwa kwa Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sherehe za uapisho zimefanyika katika Uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu, Dodoma leo tarehe 3 Novemba 2025, na kuhudhuriwa na Marais na Viongozi wa Mataifa mbalimbali, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, Wawakilishi wa Jumuiya na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi Wakuu wa Kitaifa pamoja na mamia ya Watanzania.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)


.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)


