ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua tena Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla kushika wadhifa wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo tarehe 06 Novemba 2025 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A. Said, uteuzi huo umeanza rasmi tarehe hiyo hiyo.
Aidha,taarifa hiyo imeeleza kuwa, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ataapishwa siku ya Jumamosi, tarehe 08 Novemba 2025, saa 4:00 asubuhi katika Ikulu ya Zanzibar.

