DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliofanyika leo tarehe 14 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Bunge hilo la 13 limezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kulihutubia kwa kuweka mwelekeo wa Serikali katika kipindi cha pili cha utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Viongozi Waastafu SMT na SMZ, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wastaafu na walioko madarakani, Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini na Wageni waalikwa.












.jpg)





