Rais Dkt.Mwinyi ateta na Makamu wa Rais Dkt.Nchimbi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, aliyefika Ikulu kujitambulisha leo Novemba 22,2025.
Rais Dkt. Mwinyi amempongeza kwa kushika wadhifa huo na kumhakikishia ushirikiano wa kiwango cha juu katika utekelezaji wa masuala yanayohusu Muungano.
Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa mafanikio makubwa yamefikiwa katika kuzipatia ufumbuzi changamoto nyingi zilizokuwepo awali, hivyo juhudi zinapaswa kuendelezwa ili kuimarisha Muungano kwa maslahi ya pande zote mbili.
Naye Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa ushindi mkubwa wa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na kuelezea matumaini yake ya kuiona Zanzibar ikifanya maendeleo makubwa zaidi katika miaka mitano ijayo.
Akizungumzia Muungano, ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza dhamira thabiti ya kuufanya Muungano kuwa imara zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news