Rais Dkt.Mwinyi ateua Baraza la Mawaziri

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa, uteuzi wa Mawaziri wateule unalenga kuimarisha kasi ya maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nane.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Sambamba na kuhakikisha huduma kwa wananchi zinatolewa kwa ufanisi na uwazi, huku akiwasisitiza weledi, uadilifu na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

Katika kutangaza uteuzi huo, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakuwa na jumla ya wizara 20 badala ya 18 zilizokuwepo katika kipindi cha kwanza, ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi katika kusimamia sekta mbalimbali Serikalini.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo 13,Novemba 2025, Ikulu Zanzibar, katika hafla ya kuwatangaza Mawaziri wateule. 

Hafla hiyo imehudhuliwa na Waandishi wa Habari na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Akitangaza Mawaziri na Naibu Mawaziri hao wateule, Dkt. Mwinyi ameyataja majina yao pamoja na Wizara watakazoongoza kama ifuatavyo:

MAWAZIRI

DKT. HAROUN ALI SULEIMAN, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

MHE. DKT. SAADA MKUYA SALUM, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu

MHE. DKT. JUMA MALIK AKIL, Waziri wa Fedha na Mipango

MHE. IDRISSA KITWANA MUSTAFA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,

Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

MHE. SHARIFF ALI SHARIFF, Waziri wa Kazi na Uwekezaji

MHE. HAMZA HASSAN JUMA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi

MHE. RAHMA KASSIM ALI, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

MHE. LELA MUHAMED MUSSA, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali

MHE. SHAABAN ALI OTHMAN, Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji

MHE. SULEIMAN MASOUD MAKAME, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo

MHE. NADIR ABDULLATIF ALWARDY, Waziri wa Maji, Nishati na Madini

MHE. MASOUD ALI MOHAMED, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi

MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

MHE. ANNA ATHANAS PAUL, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MHE. MUDRIK RAMADHAN SORAGA, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu

MHE. RIZIKI PEMBE JUMA, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo


NAIBU MAWAZIRI

MHE. BADRIA ATAI MASOUD, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

MHE. DKT. HAMAD OMAR BAKARI, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango

MHE. ALI ABDULGULLAM HUSSEIN, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

MHE. ZAWADI AMOUR NASSOR, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MHE. SALHA MOHAMED MWINJUMA, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

MHE. SEIF KOMBO PANDU, Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini

MHE.DKT.SALUM SOUD HAMID, Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo

MHE. MBOJA RAMADHAN MSHENGA, Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi

MHE. MOHAMED SIJAMINI MOHAMED, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu

MHE. HASSAN KHAMIS HAFIDH, Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji

MHE. KHADIJA SALUM ALI, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali


Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa,nafasi za Wizara nne ameziacha wazi kwa muda, hadi Serikali ikamilishe makubaliano na Chama cha ACT Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Wizara zilizoachwa wazi:

-Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais

-Wizara wa Afya.



Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, uteuzi huo umezingatia uwiano wa kijinsia, uwakilishi wa pande zote mbili za Unguja na Pemba, pamoja na uzoefu wa viongozi katika sekta husika.

Katika kuzungumzia mwelekeo wa Serikali, Dkt. Mwinyi amesema Zanzibar inaingia kwenye zama za uchumi wa kidijitali, na hivyo Serikali itaendelea kuwekeza katika mifumo ya kisasa, teknolojia, na kuongeza kasi ya utendaji kazi kwa ubunifu na bidii.

Ameongeza kuwa, Serikali itaweka mfumo wa tathmini ya utendaji kazi kwa lengo la kubaini iwapo viongozi wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, sambamba na kuhakikisha uwajibikaji unazingatiwa katika utumishi wa umma.

Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya Jumamosi tarehe 15 Novemba 2025 kuanzia saa 8:00 mchana, Ikulu, Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news