DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 14 Novemba 2025 anatarajiwa kumuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa ya Ikulu imesema kuwa hafla ya uapisho itafanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma kuanzia saa 10:00 asubuhi.
Uteuzi wa Dkt. Mwigulu umefanyika baada ya jina lake kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 13, 2025.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mwigulu alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango. Anachukua nafasi ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye amehitimisha kipindi cha miaka 10 cha utumishi wake kama Waziri Mkuu.

