ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewateua viongozi wapya nane kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Novemba 6, 2025 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A. Said.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 06 Novemba 2025, na viongozi hao wanatakiwa kuripoti katika Baraza la Wawakilishi kesho tarehe 07 Novemba 2025.

