ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi atalihutubia Baraza la 11 la Wawakilishi Zanzibar kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Nane, kesho tarehe 10 Novemba 2025 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi-Chukwani.
