DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Mheshimiwa Joel Nanauka kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana.
Uteuzi huo umetangazwa leo, Oktoba 17, 2025, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, wakati Rais Samia akilitangaza rasmi Baraza jipya la Mawaziri. Mawaziri walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa kesho.
