NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza Baraza jipya la Mawaziri leo huku akifanya mabadiliko makubwa ambayo yamewaondoa baadhi ya mawaziri waliokuwepo kwenye baraza lililopita.

Katika mabadiliko hayo, jumla ya mawaziri saba hawajapangiwa tena majukumu kwenye baraza jipya licha ya kuhudumu katika nafasi hizo kwenye kipindi kilichotangulia.Mawaziri waliowekwa pembeni na na nafasi zao ni pamoja na:
1:Dkt. Doto Biteko (Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati).
2:Hussein Bashe (Waziri wa Kilimo).
3:Innocent Bashungwa (Waziri wa Mambo ya Ndani).
4:Jenista Mhagama (Waziri wa Afya).
5:Dkt.Seleman Jafo (Waziri wa Viwanda na Biashara).
6:Dkt.Pindi Chana (Waziri wa Maliasili na Utalii).
7:Dkt.Damas Ndumbaro (Waziri wa Katiba na Sheria).Soma kwa kina hapa》》》