NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Tume Huru ya Uchunguzi ya Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania Mohamed Chande Othman katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume hiyo, Ikulu Chamwino, tarehe 20 Novemba, 2025.Halikadhalika, alisema Tume itapatiwa hadidu za rejea ikiwemo uchunguzi wa kina wa chanzo cha matukio hayo, mienendo ya wadau mbalimbali wa siasa na jamii, pamoja na hatua zilizochukuliwa kukabiliana na vurugu hizo na mazingira yaliyohatarisha amani na kusababisha madhara kwa wananchi na Serikali.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa pamoja na Wajumbe wa Tume hiyo kabla ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2025.Rais Dkt. Samia aliunda Tume hiyo tarehe 18 Novemba, 2025 kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi ya mwaka 2023 (Sura ya 32). Tume itakuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, na imepewa muda wa miezi mitatu ya utekelezaji wa jukumu hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Rais Dkt. Samia amewashukuru wajumbe wa Tume kwa kukubali jukumu hilo muhimu kwa maslahi ya Taifa na kusisitiza kuwa ana imani na uwezo wao wa kulitekeleza jukumu hili kubwa kwa weledi na uadilifu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2025 kabla ya kuzindua Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.Katika hatua nyingine, alisisitiza kuwa kazi na mapendekezo ya Tume hiyo yataweka msingi kuelekea uundwaji wa Tume ya Mazungumzo na Maridhiano kama alivyoahidi kuiunda katika siku 100 za mwanzo za muhula wa pili wa uongozi wake.
Tags
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Tume Huru ya Uchunguzi
Uchunguzi
Uvunjifu wa Amani
Vurugu Uchunguzi Mkuu





