NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni wafuatao:-
(i) Bi. Jenifa Christian Omolo, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Maendeleo ya Vijana. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Omolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha; na
(ii) Dkt. Kedmon Elisha Mapana, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Mapana alikuwa Katibu Mtendaji, Baraza la Sanaa la Taifa.
Aidha, uapisho wa viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 21 Novemba, 2025 saa 8.00 mchana.