ABUJA-Rais wa Nigeria, Mheshimiwa Bola Ahmed Tinubu ametangaza hali ya dharura ya usalama wa kitaifa katikati ya ongezeko kubwa la mashambulizi ya mauaji na utekaji nyara wa watu wengi katika majimbo kadhaa nchini humo.

Katika agizo lenye maneno makali lililotolewa Novemba 26,2025, Rais huyo ameamuru kuongezwa haraka kwa vikosi vya usalama wa nchi na hatua kali kuchukuliwa kukabiliana na kile alichokiita mawakala wa uovu wanaodhoofisha taifa.
Kwa mujibu wa amri mpya, Jeshi la Polisi la Nigeria lazima liongeze maafisa wengine 20,000 na kuongeza jumla ya idadi iliyopangwa hadi 50,000.
Aidha,Rais pia aliidhinisha matumizi ya kambi za National Youth Service Corps (NYSC) kama vituo vya mafunzo vya muda ili kuharakisha kupelekwa kwao kuanza majukumu.

