Taarifa muhimu kutoka TRC kwa abiria waliokata tiketi Oktoba 30,2025

DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza upya safari za treni kwa abiria waliokata tiketi Oktoba 30,2025 kati ya Morogoro na Dar es Salaam na Dar es Salaam na Dodoma kama ifuatavyo;
Safari ya Morogoro hadi Dar

Mpendwa Abiria, Shirika la Reli Tanzania linapenda kukutaarifu abiria uliekata tiketi kuelekea Dar Es Salaam kupitia Morogoro kwa tarehe 30/10/2025 hadi 05/11/2025. Safari imepangwa kufanyika tarehe 05/11/2025 saa 11:15 Alfajiri.

Tunaomba uthibitishe safari yako mapema ili kupata nafasi kwa kutuma ujumbe mfupi(sms) kwenda namba 0738594962 au piga simu 0800110042.

Aidha, kama umepanga kusafiri kwa tarehe tofauti na tarehe 5/11/2025 tunaomba kupata taarifa ya safari ya tarehe husika. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Safari ya Dodoma

Mpendwa Abiria, Shirika la Reli Tanzania linapenda kukutaarifu abiria uliekata tiketi kuelekea Dodoma kwa tarehe 30/10/2025 hadi 05/11/2025. Safari imepangwa kufanyika tarehe 05/11/2025 saa 2:00 Asubuhi.

Tunaomba uthibitishe safari yako mapema ili kupata nafasi kwa kutuma ujumbe mfupi(sms) kwenda namba 0738594962 au piga simu 0800110042.

Aidha, kama umepanga kusafiri kwa tarehe tofauti na tarehe 5/11/2025 tunaomba kupata taarifa ya safari ya tarehe husika. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news