KIJANA kutoka Shinyanga Mjini, Peter Alex Frank, maarufu kwa jina la Mr. Black, amejitosa rasmi kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mr. Black amechukua na kurejesha fomu Novemba 4, 2025, katika Makao Makuu ya CCM Taifa, Dodoma, hatua inayomweka kwenye orodha ya watia nia wanaowania nafasi hiyo muhimu ya uongozi wa chombo cha kutunga sheria nchini.
Akiwa kijana pekee miongoni mwa watia nia waliorejesha fomu hadi sasa, Mr. Black amesema uamuzi wake unatokana na dhamira ya dhati ya kutumia uwezo alio nao katika kulinda na kusimamia kanuni, sheria na taratibu za Bunge, pamoja na kuhamasisha utendaji na uchapakazi wa wabunge katika majimbo yao.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










