Tanzania,ardhi salama ambayo kila mtalii ana ndoto ya kufika

MASHIRIKA makubwa na maarufu ya ndege duniani kama Qatar na KLM yameendelea kupata abiria wengi wanaofanya safari zao kuja Tanzania kwa lengo kubwa moja tu la kutimiza ndoto za maisha yao kufika na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.
Haya yanaendelea kudhihirika kwa wingi wa wageni wanaoendelea kuingia nchini, mathalani, mnamo tarehe 20 na 21 Novemba 2025, Mamia ya watalii waliwasili nchini wakitokea nchi mbalimbali duniani kupitia ndege za mashirika ya Qatar na KLM.
Wengi wao wakieleza shauku zao za kupanda Mlima Kilimanjaro ambao wamekuwa wakisikia sifa zake kwa miaka mingi maishani mwao.
Wengi wanapofika nchini huvutiwa zaidi na hali ya amani na utulivu pamoja na watu waliojaa utu na ukarimu wa hali ya juu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news