DAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha kwa makubaliano ya pande mbili mkataba wa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco.
Kutokana na hatua hiyo, TFF imemteua Kocha Miguel Gamondi wa Singida Black Stars kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars.
Mazungumzo kati ya TFF na Singida Black Stars tayari yamekamilika ili kuhakikisha kocha huyo anachukua majukumu mapya kwa utaratibu mzuri.
Kocha Gamondi ndiye atakayeiongoza Taifa Stars kwenye Fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba mwaka huu.


Tags
Breaking News
Habari
Hemed Suleiman morocco
Michezo
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Taifa Stars
.jpeg)