ZANZIBAR-Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza uteuzi wa Wajumbe wa Viti Maalum vya Wanawake katika Baraza la Wawakilishi kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Uteuzi huo umefanyika tarehe 04 Novemba 2025 katika kikao maalum cha tume.
Uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa kifungu cha 67(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na kifungu cha 55(3) cha Sheria ya Uchaguzi Na. 4 ya mwaka 2018.
Uteuzi huo umefanyika chini ya masharti ya kifungu cha 67(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu cha 55(3) cha Sheria ya Uchaguzi Nam. 4 ya mwaka 2018. Wajumbe walioteuliwa ni wafuatao:-
1) Ndg. Zainab Khamis Shomari - CCM
2) Ndg. Rahma Kassim Ali - CCM
3) Ndg. Tabia Maulid Mwita - CCM
4) Ndg. Fatma Ramadhan Mandoba - CCM
5) Ndg. Riziki Pembe Juma - CCM
6) Ndg. Maryam Said Khamis - CCM
7) Ndg. Chumu Khamis Kombo - CCM
8) Ndg. Lela Muhamed Mussa - CCM
9) Ndg. Khadija Salum Ali - CCM
10) Ndg. Zainab Abdalla Salum - CCM
11) Ndg. Anna Athanas Paul - CCM
12) Ndg. Aza January Joseph - CCM
13) Ndg. Salha Moh'd Mwinjuma - CCM
14) Ndg. Hudhaima Mbarak Tahir - CCM
15) Ndg. Mwanaidi Kassim Mussa - CCM
16) Ndg. Salma Mussa Bilali - CCM
17) Ndg. Moza Mohamed Khamis - ACT Wazalendo
18) Ndg. Jabu Makame Juma - ACT Wazalendo
19) Ndg. Farida Amour Mohamed - ACT Wazalendo
20) Ndg. Nassra Nassor Omar - ACT Wazalendo
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeteuwa Wajumbe 16 kutoka CCM na Wajumbe wanne kutoka ACT Wazalendo kunatokana na asilimia ya viti vya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walivyopata katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba,2025.

