DODOMA-Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuutarifu umma kuwa, kwa mujibu wa kalenda ya kitaaluma ya mwaka wa masomo 2025/2026, vyuo vyote vya elimu ya kati na ya juu, vya umma na binafsi, vitafunguliwa kama ifuatavyo:
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanatakiwa kuripoti vyuoni kwa ajili ya programu ya utangulizi (orientation programme) kuanzia Novemba 17, 2025, kabla ya kuanza rasmi kwa masomo.
Wanafunzi wanaoendelea watarudi vyuoni kuanza rasmi masomo kuanzia Novemba 24, 2025.
Wizara inawahimiza wanafunzi wote kuhakikisha wanawasili vyuoni kwa wakati, kufuata ratiba zilizopangwa, na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kitaaluma.
