MOROGORO-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji, akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, wamewasili mkoani Morogoro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Kijaji na Mhe. Chande wanatarajiwa kutembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Lengo la ziara hii ni kujifunza, kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii pamoja na kujitambulisha katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Tags
Dr Ashatu Kijaji
Habari
Viongozi wa Maliasili na Utalii Tanzania
Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania





