MANYARA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imetoa elimu kinga juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Uhasibu (IAA) Kampasi ya Babati mkoani Manyara.

Elimu hiyo iliyotolewa katika program ya Orientation ilikazia uhusiano wa Rushwa na Dawa za Kulevya.
Pia, wanafunzi walihamasishwa kutojihusisha na dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)


