Azam FC yaacha huzuni na majonzi Simba SC kwa mabao 2-0

NA DIRAMAKINI

AZAM FC ya jijini Dar es Salaam imesababisha huzuni na majonzi kwa mashabiki wa Simba Sports Club (Simba SC) baada ya kuichapa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Ni kati ya matokeo ambayo yameendelea kutonesha kidonda baada ya kukumbana na kipigo katika mechi mbili mfululizo ikiwemo bao 1- 0 dhidi ya Petro de Luanda na kupoteza tena kwa mabao 2-1 mbele ya Stade Malien michuano ya CAF Champions League 2025/26.

Kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo Desemba 7,2025 ulikuwa wa vuta nikuvute huku kila timu ikionesha uwezo mkubwa wa kutaka alama tatu muhimu.

Azam FC ilipata mabao yote kipindi cha pili kupitia kwa Jephte Kitambala dakika ya 81 na Iddy Seleman ‘Nado’ dakika ya 88.

Ushindi huo wa mabao mawili umeongeza hamasa kwa mashabiki wa Azam FC ambao wamekuwa wakitoa sapoti kubwa kwa timu yao msimu huu.
Aidha,mashabiki hao wanaamini matokeo haya
yanaimarisha nafasi ya klabu hiyo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa Simba SC, matokeo haya yameiacha katika wakati mgumu kwa michuano ya ndani na Kimataifa.

Aidha, wanaendelea kusalia katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania ikiwa na alama 12 baada ya mechi tano, huku Azam FC wakiwa nafasi ya tisa kwa alama tisa baada ya mechi tano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news