NA DIRAMAKINI
BAO pekee la Prince Dube limeongeza hamasa kubwa na hari ya kusonga mbele kwa Young Africans Sports Club (Yanga SC) katika michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Dube aliwainua mshabiki wa Yanga SC dakika ya 89 kwa kufunga bao safi la kichwa dhidi ya Coastal Union akitumia krosi ya Duke Abuya.Mtanange huo umepigwa leo Desemba 7,2025 katika dimba la Jamhuri lililopo katika makao makuu ya nchi jijini Dodoma.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC imesogea nafasi ya pili ikiwa na alama 16, baada ya kucheza michezo sita, huku watani zao Simba SC wakiwa nafasi ya tano wakiwa na alama 12, baada ya kucheza michezo mitano.