Slovakia yafungua Ubalozi nchini Tanzania

DODOMA-Balozi Mteule wa kwanza wa Slovakia nchini Tanzania, Mhe. Ivan Lančarič amewasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe jijini Dodoma leo Desemba 10, 2025.
Mhe. Lančarič amewasilisha Nakala hizo za Hati za Utambulisho kufuatia nchi yake kufungua Ubalozi nchini Mwezi Desemba 2025.
Akipokea Nakala za Hati hizo, Mhe. Maghembe amesema ufunguzi wa Ubalozi huo ni matokeo ya utekelezaji uliotukuka wa Diplomasia ya Tanzania duniani, chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Ubalozi huu utakuwa kichocheo cha kukuza ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Slovakia, hususan katika nyanja za uwekezaji, biashara na utalii,"Dkt. Maghembe alisema.

Kwa upande wake, Mhe. Lančarič alieleza ufunguzi wa ubalozi mpya nchini Tanzania ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, ambayo inalenga kutanua wigo wa uwakilishi barani Afrika.
Alisema Ubalozi huo utawakilisha sio tu Tanzania bali nchi nyingine za Afrika kama vile Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Congo Brazzaville, Burundi, Gabon, Cameroon na Guinea ya Ikweta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here