NA DIRAMAKINI
UONGOZI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba na Meneja Mkuu Dimitar Pantev pamoja na Wasaidizi wake wawili.
Kwa sasa kikosi kitabaki chini ya Kocha Selemani Matola wakati mchakato wa kutafuta kocha mwingine unaendelea.

