Dkt.Natu El-Maamry Mwamba atembelea jengo jipya la ofisi za Wizara ya Fedha

NA SAIDINA MSANGI
WF

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ametembelea Jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma, ambapo amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo la kisasa linalotarajiwa kuwa ‘State of the Art’.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akiongozwa na Msimamizi wa Mradi Bw. Hija Mrutu, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akisikiliza taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Msimamizi wa Mradi, Bw. Hija Mrutu, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.

Dkt. Mwamba aliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda na Msimamizi wa Mradi Bw. Hija Mrutu na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha, kutembelea Ofisi mbalimbali ndani ya Jengo hilo na kujionea kazi kubwa iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akisajiliwa kwa kutumia mfumo wa vitambulisho wa kielektoniki na Afisa Tehama Wizara ya Fedha, Bw. Omary Waziri, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.

Dkt. Mwamba alipongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo hilo na kueleza kuwa zoezi la ukamilishaji wa uwekaji wa Samani litakapo kamilika watumishi wote watahamia kwenye Jengo hilo na kwamba hivi sasa baadhi ya Idara zimehamia katika Jengo Hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Menejimenti wa Wizara ya Fedha, baada ya kukamilisha zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.
Mwonekano wa maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Alisema Ofisi alizotembelea zina utulivu wa kutosha kuweza kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika mazingira bora na rafiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news