Hatutaki watumishi wa Sekta ya Ardhi kuwa sehemu ya matatizo-Dkt.Akwilapo

MASASI-Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt.Leonard Akwilapo amesema wizara yake haitaki watumishi wa sekta ya ardhi kuwa sehemu ya migogoro ya ardhi nchini.
Mhe. Dkt.Akwilapo ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Desemba 2025 wilayani Masasi wakati alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
"Kuanzia sasa hatutaki mtumishi wetu awe sehemu ya tatizo tukigundua wewe mtumishi wa sekta ya ardhi umekuwa sehemu ya tatizo basi wewe siyo mfanyakazi wetu na hilo tutalisimamia,"amesema.
Amebainisha kuwa, matatizo ya ardhi yapo na yanatengenezwa na watumishi wa sekta ya ardhi pamoja na wananchi ambapo ameweka wazi kuwa, matatizo yaliyotengenezwa basi wizara yake itayatatua.

"Hatupendi kufukuza kazi watumishi maana tunajua kila mfanyakazi anategemewa na kumfukuza itakuwa kitu cha mwisho lakini kuna mahali inabidi sheria ifuate mkondo wake.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo yupo wilayani Masasi mkoa wa Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na wananchi wa jimbo lake kwa lengo la kusikiliza na kizitafutia ufumbuzi changamoto mablimbali jimboni humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news