Serikali yaahidi kuendeleza ushirikiano na UNICEF kuimarisha maendeleo ya huduma za jamii nchini

NA JOSEPH MAHUMI
WF

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo, ambapo wamejadili kuhusu namna ya kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na shirika hilo hususan maendeleo ya huduma za jamii.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (Kulia), akiwa na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo, walipokutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika hilo hasa katika kutekeleza miradi inayolenga kuinua ustawi wa jamii na kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati alipokutana na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo (hayupo pichani), ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.
Dkt. Mwamba alisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na UNICEF katika kutekeleza miradi inayolenga kuinua ustawi wa jamii na kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.

Kwa upande wake, Bi. Patricia Safi Lombo, aliyefika kujitambulisha, Treasury Square jijini Dodoma, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua kubwa ilizopiga katika kusimamia sekta za kijamii, na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu zaidi katika utekelezaji wa programu za maendeleo zenye tija kwa watoto.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (Watatu kulia) na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo (wa nne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha pamoja na UNICEF, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, Ofisi za Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalihitimishwa kwa pande zote mbili kueleza nia ya kuimarisha zaidi uhusiano uliopo, kupitia mipango bunifu inayochochea ustawi wa watoto, vijana na jamii kwa ujumla, sambamba na malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news