Jeshi la Polisi lafuatilia taarifa za kutoweka kwa Mtawa mkoani Morogoro

MOROGORO-Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linafuatilia taarifa za kutoweka kwa Mtawa aliyetambulika kwa jina la Silianus Korongo (49) Mkazi wa Mtaa na Kata ya Tungi, Manispaa ya Morogoro, ambaye ametoweka katika nyumba ya malezi ya Watawa wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Franciscan (ORDER OF FRIARS MINOR -OFM ) tangu Disemba 1, 2025.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, aliyoitoa Disemba 3, 2025 imeeleza kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa za kutoweka kwa Mtawa huyo, ikieleza kwamba mara ya mwisho alitoka kwa ajili ya kwenda kununua Vifaa vya Ujenzi na hakurejea.

Kamanda Mkama amesema uchunguzi na ufuatiliaji unaendelea, huku Jeshi hilo likitoa wito kwa Mwananchi yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kuhusu kutoweka kwa Mtawa huyo kuwasilisha taarifa hizo katika kituo chochote cha Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here