DAR-Maafisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam wamekutana katika kikao cha pamoja na Brigedia Jenerali Justus Mwilambeghe Kitta wa Kikosi cha 302 KV cha Jeshi la Wananchi Tanzania.
Katika kikao hicho wamekumbushana umuhimu wa ushirikano, kuendeleza uzalendo wa kulilinda Taifa, nidhamu, weledi na mawasiliano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kujenga taswira ya vyombo hivyo vizidi kun’gara na kuwa tegemeo kwa Taifa na wananchi kwa ujumla.
Hayo yamezungumzwa leo Desemba 30, 2025 wakati Brigedia Jenerali Justus akiwa na SACP Muliro Muliro,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
Kamanda Muliro amemshukuru Brigedia Jenerali Kitta na ujumbe wake kwa kumtembelea Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.


