WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi amesema kuwa katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka 2024 yaliyofanyika mkoani Ruvuma, Serikali ilisambaza matokeo ya utafiti wa hali ya VVU na Ukimwi nchini ambayo yanaonesha kuwa takribani watu milioni 1.7 wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Ukimwi Duniani, Lukuvi alisema matokeo hayo pia yanaonesha mafanikio katika upatikanaji wa huduma za VVU na Ukimwi, ikiwamo ongezeko la watu wanaotambua hali zao za maambukizi kutoka asilimia 91 mwaka 2024 hadi asilimia 92 mwaka huu.Aidha, amesema kiwango cha watu wanaoishi na VVU (WAVIU) wanaotumia dawa za kufubaza virusi (ARV) kimeongezeka kutoka asilimia 98 mwaka 2024 hadi asilimia 98.5 mwaka huu, hatua aliyoielezea kuwa ni ishara ya kuimarika kwa huduma za afya kwa watu wanaoishi na VVU.






















Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










