RAIS wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amezindua rasmi Uwanja wa Hoima City wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000, sehemu ya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, litakaloandaliwa kwa pamoja na Uganda, Kenya na Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Museveni alisema maendeleo yanayoendelea nchini Uganda ni matokeo ya sera za kimapinduzi, akitolea mfano mafanikio ya kampuni ya Kira EV inayotengeneza mabasi ya umeme, ambayo tayari imepokea oda ya mabasi 450 hadi Afrika Kusini.
Rais pia alisema Uwanja wa Hoima City ni mojawapo ya miradi 10 ya kimkakati inayotekelezwa kwa ajili ya maandalizi ya AFCON 2027, akipongeza kampuni ya Kituruki Summa kwa kazi nzuri ya ujenzi na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika miradi mingine ya maendeleo.










Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




