Katibu wa Kamati ya Mapinduzi Cup, Rashid Said Suleiman, amesema kuwa moja ya vigezo muhimu kwa timu kushiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi ni lazima iwe timu ya Ligi Kuu, hususan kutoka Tanzania Bara au Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 27, 2025, kuelekea ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026 utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan New Complex, jijini Zanzibar, Suleiman amesema kuwa mbali na mshindi kupewa Kombe la Mapinduzi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, atatoa zawadi ya fedha kwa mshindi wa kila mechi kupitia Mfuko wa Rais wa Zanzibar.
Aidha, jumla ya klabu 10 zimepangwa kushiriki michuano hiyo ya msimu huu, ambapo zimegawanywa katika makundi matatu. Kundi A linajumuisha Mlandege, Azam FC, Singida Black Stars na URA ya Uganda. Kundi B lina Simba, Mwembe Makumbi na Fufuni, huku Kundi C likiwa na Yanga, TRA United na KVZ.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi msimu huu inatarajiwa kuanza Jumapili na itafikia tamati Januari 13, 2026, siku moja baada ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12,1964.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















