Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imewekea historia Tanzania, Afrika Mashariki na Kati kwa kutoa matibabu mapya ya tiba ya kupunguza msisimko wa shinikizo la damu katika mishipa ya figo (Renal denervation therapy).

Matibabu hayo ambayo yameanza kutolewa leo katika Taasisi hiyo yanatolewa kwa wagonjwa wenye matatizo ya shinikizo la juu la damu la muda mrefu ambalo halishuki kwa matibabu ya dawa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














