Miongozo ya kukabiliana na maafa nchini yapitishwa

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Kamati ya Wataalam ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa leo 19 Desemba,2025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome, jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, Mpango wa Taifa wa- dharura wa kukabiliana na Ukame, Mafuriko na Majanga mengine yanayohusiana kwa kipindi cha Novemba 2025 hadi Juni 2026 umejadiliwa na kupokelewa na wajumbe wa kikao.

Aidha, Miongozo ya uanzishwaji na Uendeshaji wa kituo cha operesheni na Mawasiliano ya dharura na Timu ya kukabiliana na Dharura ngazi ya Taifa na Mkoa imejadiliwa na kupitishwa na wajumbe wa kikao.
Miongozo iliyojadiliwa na kupitishwa ni pamoja na, Mwongozo wa Uanzishaji wa kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Mwongozo wa Uendeshaji wa kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ngazi za Mikoa, Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Timu ya Mkoa ya kukabiliana na Dharura.

Pia, Muongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Timu ya Taifa ya kukabiliana na Dharura, Muongozo wa Uendeshaji wa Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Muongozo wa kuandaa Mpango wa Mkoa wa kujiandaa na kukabiliana na Maafa.
Pamoja na hayo, Wajumbe wa kikao hicho walipokea na kuridhia Mkakati wa Utekelezaji wa Mpango wa Utoaji wa Huduma za Tahadhari ya mapema kwa wote kwa kipindi cha miaka Mitano (2026-2030).

Awali, Dkt.Yonazi ametoa pongezi kw taasisi na sekta mbalimbali zinazokabiliana na Maafa kwa kuendelea kufanya vizuri na kutoa elimu ya maafa nchini na nchi jirani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here