Nyuki Marathon yavuka mipaka

ARUSHA-Mashindano ya Riadha yanayojali Mazingira ya Arusha ya Nyuki Marathon (Bees Marathon) yamevuka mipaka hadi nchini Zimbabwe ambapo msimu wa tatu wa Mashindano ya kila mwaka utafanyika nchini humo na yamepangwa kufanyika Mei 2026.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Worker Bees Africa ili kukuza ulinzi na uhifadhi wa nyuki, yanatumia fursa hiyo pia kuongeza ufahamu kuhusu Kongamano lijalo la Global Apimondia linalotarajiwa kufanyika Septemba 2027.

Tume ya Michezo na Burudani ya Zimbabwe imesaini Mkataba maalum wa Makubaliano (MoU) na Worker Bees Africa ili kuwezesha kufanyika kwa mbio za Nyuki Marathon katika nchi hiyo iliyopo Kusini mwa Afrika.

Rais wa Apimondia Kanda ya Afrika, David Mukomana ni mmoja wa watia saini wa MoU alisema anafurahi kwamba mashindano ya Mbio hatimaye yanaenda kufanyika nchini Zimbabwe kwani imekuwa ndoto yake siku zote.

Kwa mujibu wa Mukomana nchi zisizopungua tisa tayari zimethibitisha ushiriki wao wa Nyuki Marathon 2026 zikiwemo Uganda, Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Lesotho, Botswana, na Malawi huku baadhi ya wakimbiaji walioko Australia, Canada na Uingereza pia wakionyesha nia ya kujiunga na mbio hizo nchini Zimbabwe.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Michezo na Burudani, Peter Mudzimiri amesema mbio za Nyuki Marathon, mbali na kusaidia uhifadhi, pia zitasaidia juhudi zinazoendelea za kukuza sekta ya michezo na burudani nchini Zimbabwe.

Nyuki Marathon 2026 itashirikisha makundi manne ya mbio zikiwemo mbio kamili za kilomita 42, mbio na nusu za kilomita 21, mbio za kilomita 10 na mbio fupi zaidi za kilomita 5 ambazo ni mbio za kujifurahisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news