Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika mazishi ya Fadya Abdalla Seif

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi na wananchi mbalimbali katika mazishi ya Bi.Fadya Abdalla Seif aliyefariki dunia leo Disemba 30,2025.
Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza iliyosaliwa Masjid Jamiu Zinjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Marehemu Bi. Fadya Abdalla Seif ni mama mzazi wa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, ndugu Arif Abdalla Manji. Marehemu amezikwa kijijini kwao Kazole, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here