ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo Disemba 30, 2025 amemteua ndugu Makame Hasnuu Makame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme, Zanzibar (ZECO).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Kabla ya mabadiliko, ndugu Makame alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA).
Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Sultan Said Suleiman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA).
Kabla ya mabadiliko, ndugu Sultan alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Pia,Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua tena Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPDC).
Dkt.Abdulhamid ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

.jpg)