ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha Wakuu wa Mikoa na Manaibu Makatibu Wakuu aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya uapisho imefanyika leo tarehe 17 Disemba 2025 Ikulu, Zanzibar.
Walioapishwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo, na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mhe. Muhammed Ali Abdalla.
Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa ni Ndg. Hawaah Ibrahim Mbaye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu, pamoja na Dkt. Said Seif Mzee, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.


















