LINDI-Mkuu wa Kitengo cha Sera, Mipango na Bajeti toka Kamisheni ya Fedha na Lojistiki Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Rashidi ngonyani akiwa ameambatana na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Emmanuel Rioba amefanya kikao kazi na Makanda wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa lengo la kutoa elimu kwa ajili ya uandaaji wa bajeti kulingana na mpango wa Jeshi la Polisi kwa mwaka 2026/2027.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Lindi ambapo mkoa wa Mtwara uliwakilishwa na Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Polisi (SACP) Issa Suleiman, mkoa wa Lindi kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) John Imori na mkoa wa Ruvuma ni Afisa Mnadhimu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Alfred Hussein, maafisa Waandamizi pamoja na wahasibu wa Polisi wa mikoa hiyo.






