Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky afanya mazungumzo na Papa Leo XIV

NA DIRAMAKINI

Viongozi hao wamekutana Desemba 9,2025 ambapo katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamejadili kwa kina njia za kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Ukraine, kufuatia vita inayoendelea kati ya Ukraine na Urusi ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.

Aidha,mazungumzo hayo pia yamegusia umuhimu wa mshikamano wa kimataifa katika kusimamia haki, utu wa binadamu na maelewano ya kidiplomasia kwa ajili ya ustawi wa raia wa Ukraine na dunia kwa ujumla.

Vilevile, Rais Zelenskyy amemualika Papa kutembelea nchi ya Ukraine akisisitiza kuwa, Taifa hilo linathamini msaada wa Papa Leo XIV na Vatican, ikiwemo misaada ya kibinadamu na utayari wa kupanua misaada hiyo nchini humo.

Pia, amemshukuru Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani kwa maombi yake ya kudumu kwa Ukraine na wito wake wa amani ya haki.
"Nilimjulisha kuhusu juhudi za kidiplomasia na Marekani, na tukajadili hatua zaidi za upatanishi za Vatican, hasa kuhusu kurejeshwa kwa watoto waliotekwa na Urusi.Nimeeleza shukrani kwa juhudi zake kwa vijana wa Ukraine na kumkaribisha kuzuru Ukraine kama ishara ya mshikamano."

The Ukraine President Volodymyr Zelensky wrote... "Ukraine deeply appreciates all the support of His Holiness Pope Leo XIV @Pontifex and the Holy See – the ongoing humanitarian assistance and the readiness to expand humanitarian missions.

"During today’s audience with His Holiness, I thanked him for his constant prayers for Ukraine and for the Ukrainian people, as well as for his calls for a just peace.

"I informed the Pope about diplomatic efforts with the United States to achieve peace. We discussed further actions and the Vatican’s mediation aimed at returning our children abducted by Russia.
"I am grateful to His Holiness for all his efforts to support young Ukrainians. Thank you for this conversation and for all the attention given to our people. I invited the Pope to visit Ukraine. This would be a powerful signal of support for our people."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news