Picha mjongeo yenye kichwa cha habari WAMASAI WAANZA MAANDAMANO KUDAI HAKI ZAO ARUSHA kama inavyoonekana kushoto mwa taarifa hii ni uzushi na uongo ipuuzeni.Ufafanuzi ni kwamba, hizo zilikuwa sherehe za Kimila za Kabila la Wamaasi za jando ambapo vijana pamoja na mambo mengine hufundishwa na kujengewa maadili.
Sherehe hizo zilifanyika mwezi Juni 2025 katika eneo la msitu wa TANAPA jijini Arusha.
Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi