Tanzania kuwafutia hadhi ya ukimbizi Wakimbizi wanaoishi nchini

DAR-Serikali ya Tanzania imesema inaenda kuwafutia hadhi ya ukimbizi Wakimbizi wanaoishi nchini baada ya kurejea kwa hali ya amani katika nchi zao baada ya hapo awali kuwepo kwa machafuko.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene huku jumla ya Wakimbizi 238,956 wanahifadhiwa hapa nchini ambapo Warundi ni 152,019,Wakongo ni 86,256 na mataifa mengine yakichangia idadi ya 681.

“Katika mkutano wa mwisho tulikubaliana kurejesha Wakimbizi 3000 kwa wiki,hata hivyo hadi tunakutana hapa hii leo 2025 ni Wakimbizi 3000 pekee waliorejea nchini kwao.

"Hili ni jambo ambalo lingepaswa kukamilika ndani ya wiki moja lakini limechukua takribani mwaka mzima,hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee hivi,"asema Waziri Simbachawene.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here