Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare wapewa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia

MARA-Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara Disemba 01,2025 wamepatiwa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia pamoja na mbinu sahihi za kuripoti matukio hayo ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Elimu hiyo imetolewa chuoni hapo na watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mara, wakiongozwa na Mkuu wa Dawati hilo, Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Benela.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Mkaguzi Benela alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia katika maeneo mbalimbali nchini, na kwamba wakati mwingine wahanga wamekuwa wakishindwa kuripoti kutokana na hofu, kutokujua utaratibu sahihi au kukosa uelewa juu ya haki zao.
Aliongeza kuwa wahanga au mashahidi wa matukio hayo hawapaswi kuwa na woga, kwani sheria inalinda taarifa na usalama wao, na vyombo vya dola vimeandaliwa kuwahudumia bila upendeleo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo waliushukuru uongozi wa chuo kwa kuandaa kikao hicho, wakisema kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kutambua dalili za ukatili wa kijinsia na namna ya kuchukua hatua mapema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news