TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa mikoa 20 nchini

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa 20 nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA leo Jumamosi Desemba 27, 2025 imetaja mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Morogoro, Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha tarehe 28 Desemba, 2025 na huenda zikasababisha madhara mbalimbali ikiwamo mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa, hususan walioko mabondeni na maeneo hatarishi, wametakiwa kuchukua tahadhari za mapema ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

TMA imewasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na utabiri wa hali ya hewa unaotolewa mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi na za wakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news