NA DIRAMAKINI
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesitishwa safari za treni ya SGR kwa muda kuanzia tarehe 31 Disemba 2025 kati ya Morogoro-Dodoma na Dodoma-Morogoro kutokana na athari za mvua zilizopelekea uharibifu wa miundombinu katika eneo la Kidete (Kilosa, Morogoro) na Godegode (Mpwapwa,Dodoma).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 31,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TRC,Mhandisi Machibya M. Shiwa
Kufuatia athari hiyo, safari zote za SGR zitakuwa kati ya Dar es Salaam-Morogoro na Morogoro-Dar es Salaam hadi pale marekebisho yatakapokamilika na usalama kuthibitishwa.
"Hivyo abiria wanashauriwa kubadili ratiba za safari zao kuendana na mabadiliko yaliyotokea. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na watalaamu wanachukua hatua za haraka ili kurejesha huduma hizi."

