Tuendelee kuiombea nchi amani na utulivu-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewanasihi viongozi wa dini na Waumini kuhimizana kulinda amani ya nchi na kuwa tayari kuiombea kwa dhamira ya kudumisha utulivu.
Dkt.Mwinyi ametoa nasaha hizo Disemba 5,2025 wakati akijumuika na Waumini katika Sala ya Ijumaa na Dua Maalum ya Kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kuliombea Taifa, iliyofanyika katika Msikiti wa Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba.

Katika hotuba yake, Dkt. Mwinyi amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia Zanzibar kuendelea kuwa na hali ya amani na utulivu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.
Amewahimiza Waumini kuendeleza maombi na dua zao kila wanapopata nafasi, akisisitiza kuwa kila Muumini ana daraja lake mbele ya Mwenyezi Mungu, hivyo ni wajibu kwa kila mmoja kumuomba Mola aiweke nchi mbali na majanga.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti, Sheikh Khalid Ali Mfaume, amewataka Waumini wa Kiislamu kuendelea kufuata miongozo ya Mtume Muhammad (SAW) kwa kumuomba Mwenyezi Mungu katika kila jambo linalowakabili katika maisha yao ya kila siku.
Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news