Uhamiaji yatangaza ajira mpya

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka niliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, natangaza nafasi za Ajira Mpya za Konstebo wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji,Dkt. Anna P. Makakala.

1. SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe ni raia wa Tanzania;

ii. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;

iii. Awe na Cheti cha Kuzaliwa;

iv. Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA);

v. Awe na siha njema ya mwili na akili.

vi. Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;

vii. Asiwe na kumbukumbu au taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;

viii. Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;

ix. Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;

x. Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na sifa kuanzia Daraja la kwanza (1) mpaka Daraja la tatu (3) na awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 22, Mwombaji mwenye Astashahada na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada/ Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka

xi. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Kijeshi ya Uhamiaji.

xii. Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.

xiii. Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la Ajira

2. MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE:

Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada/Stashahada ya Juu, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:- Mtaalamu wa Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano, TEHAMA(Cyber Security,Database Developer,System Developer,Artifical Intelligence and Machine Learning),Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa AC, Brass band, Wataalamu wa Saikolojia (Psychology) na Mpiga chapa (Printer).

Pia waombaji wenye ujuzi wa Ufundi wa Magari na Udereva watapewa kipaumbele.

3. NAMNA YA KUFANYA MAOMBI:

Maombi yote ya ajira yatawasilishwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni https://www.immigration.go.tz kuanzia tarehe 29 Desemba, 2025 na mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.

Wakati wa kufanya maombi, mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye mfumo wa ajira nyaraka zifuatazo zilizo katika mfumo wa PDF (kila Nyaraka moja isizidi 300Kb);

✓ Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png isiyozidi

300Kb kwa ajili ya kuambatisha kwenye mfumo (upload);

✓ Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono;

✓ Barua ya utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU wawe na barua za utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi;

✓ Cheti cha kuzaliwa;

✓ Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo;

✓ Awe na Index namba za vyeti vya kufaulu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ambazo atajaza kwenye mfumo wa ajira;

✓ Awe na namba ya utambuzi ya cheti cha ngazi ya Astashahada, Stashahada,na Shahada/Stashahada ya juu inayotambuliwa na TCU au NACTVET ambayo atajaza namba hiyo kwenye mfumo wa ajira;

✓ Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi;

✓ Wasifu wa mwombaji (CV).

✓ Aidha, changamoto/maulizo wasilisha kupitia: ajira@immigration.go.tz

4. TAHADHARI

(i) Maombi yote yatapokelewa katika utaratibu ulioainishwa katika kifungu Namba 3 hapo juu na si vinginevyo;

(ii) Mwombaji yoyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani;

(iii) Epuka Matapeli wanaoomba fedha au rushwa ya aina yoyote wakieleza/kudai kusaidia kupata nafasi za Ajira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news